Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Wafilipi 4:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yote, nimefundishwa kushiha na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa.

Tazama sura Nakili

Wafilipi 4:12
15 Marejeleo ya Msalaba  

Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu;

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.

NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;

Maana wasema, Nyaraka zake nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini yu dhaifu, na maneno yake hayawi kitu.

kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi.

Je! nalifanya dhambi kwa kujinyenyekea illi ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwakhubiri Injili ya Kristo bila ujira?

Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo