Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 4:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji langu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana Isa, ninyi wapendwa wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kwa hiyo, ndugu zangu, ninaowapenda na ambao ninawaonea shauku, ninyi mlio furaha yangu na taji yangu, hivi ndivyo iwapasavyo kusimama imara katika Bwana Isa, ninyi wapenzi wangu.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 4:1
35 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Kesheni, simameni imara katika Imani, mwe waume, mwe hodari.


vile vile kama mlivyotukiri kwa sehemu, ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana Yesu.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku katika moyo wake Kristo Yesu.


nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.


Kwa kuwa alikuwa na shanku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu.


BASSI wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo