Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 na kuunganishwa naye kabisa. Mimi sitaki tena uadilifu unaotokana na kuitii sheria. Sasa ninao ule uadilifu unaopatikana katika kumwamini Kristo; uadilifu utokao kwa Mungu na ambao unategemea imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 na kuunganishwa naye kabisa. Mimi sitaki tena uadilifu unaotokana na kuitii sheria. Sasa ninao ule uadilifu unaopatikana katika kumwamini Kristo; uadilifu utokao kwa Mungu na ambao unategemea imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 na kuunganishwa naye kabisa. Mimi sitaki tena uadilifu unaotokana na kuitii sheria. Sasa ninao ule uadilifu unaopatikana katika kumwamini Kristo; uadilifu utokao kwa Mungu na ambao unategemea imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nami nionekane mbele zake bila kuwa na haki yangu mwenyewe inayopatikana kwa sheria, bali ile inayopatikana kwa imani katika Al-Masihi, haki ile inayotoka kwa Mungu kupitia kwa imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nami nionekane mbele zake bila kuwa na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Al-Masihi, haki ile itokayo kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya imani.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:9
56 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.


Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hatta imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.


kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu.


Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.


illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


kwa jinsi ya haki ipatikanayo kwa sharia sikuwa na khatiya.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Killa afanyae dhambi, afanya nasi; kwa kuwa dhambi ni nasi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo