Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi aje kutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi aje kutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Lakini sisi ni raia wa mbinguni, na twatazamia kwa hamu kubwa Mwokozi aje kutoka mbinguni, Bwana Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana Isa Al-Masihi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Isa Al-Masihi,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:20
36 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


Ndivyo alivyo yeye ajiwekeae nafsi yake akiba wala hawi tajiri machoni pa Mungu.


kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.


wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


hatta hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;


Alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.


tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.


Bali Yerusalemi wa juu ni mwungwana, ndio mama yetu sisi.


Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,


akatufufua pamoja nae, akatuketisha pamoja nae katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu:


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo