Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mwisho wao ni kuangamia, kwani tumbo lao ndilo mungu wao; wanaona fahari juu ya mambo yao ya aibu, hufikiria tu mambo ya kidunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Mwisho wa watu hao ni maangamizi, mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Mwisho wa watu hao ni maangamizi, mungu wao ni tumbo, na utukufu wao ni aibu, na mawazo yao yamo katika mambo ya dunia.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:19
52 Marejeleo ya Msalaba  

Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu.


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Kiisha nitaiambia roho yangu, Ee roho yangu, nna mali nyingi ulizojiwekea akiba kwa miaka mingi: pumzika, hassi, ule, unywe, ufurahi.


Palikuwa na mtu tajiri, aliyevaa porfuro na bafuta, akafanya furaha kilia siku na anasa.


Nae hakukubali muda wa siku kadha wa kadha; khalafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa mimi simchi Mungu wala sijali mtu;


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Faida gani bassi mliyopata siku zile kwa mambo haya mnayotahayarikia sasa? kwa maana mwisho wa mambo haya ni mauti.


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Lakini nifanyalo nitalifunya, illi niwapinge watafutao nafasi wasipate nafasi; illi katika neno hilo wajisifulo waonekane kuwa kama sisi.


Bassi si neno kubwa wakhudumu wake nao wakijigeuza wawe mfano wa wakhudumu wa haki. Mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.


Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu.


Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Yesu Kristo.


Nieni yaliyo juu, siyo yaliyo katika inchi.


watakaoadhibiwa kwa uharibifu wa milele, kutengwa na uso wa Bwana na na utukufu wa nguvu zake,


illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


makhaini, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko Mungu;


Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kwote kwa namna hii ni kubaya.


LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia.


wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;


Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.


Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.


Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Kwa kadiri aliyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa alisema moyoni mwake, Nimeketi malkiya, nami si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo