Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Sisi sote tuliokomaa tunapaswa kuwa na msimamo huohuo. Lakini kama baadhi yenu wanafikiri vingine, basi, Mungu atawadhihirishieni jambo hilo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu ataliweka wazi hilo nalo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hivyo sisi sote tuliokuwa kiroho tuwaze jambo hili, hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mwenyezi Mungu ataliweka wazi hilo nalo.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu?


Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


Nina matumaini kwenu katika Bwana, kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anaewafadhaisha atachukua hukumu yake awae yote.


Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo