Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, nimo mbioni kuelekea lengo langu, ili nipate lile tuzo, ambalo ni mwito wa Mungu kwa maisha ya juu kwa njia ya Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:14
20 Marejeleo ya Msalaba  

Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto.


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi;


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo