Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Sijidai kwamba nimekwisha faulu au nimekwisha kuwa mkamilifu. Naendelea kujitahidi kupata lile tuzo ambalo kwalo Kristo amekwisha nipata mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Sijidai kwamba nimekwisha faulu au nimekwisha kuwa mkamilifu. Naendelea kujitahidi kupata lile tuzo ambalo kwalo Kristo amekwisha nipata mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Sijidai kwamba nimekwisha faulu au nimekwisha kuwa mkamilifu. Naendelea kujitahidi kupata lile tuzo ambalo kwalo Kristo amekwisha nipata mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Si kwamba nimekwisha kufikia, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha! Bali nakaza mwendo ili nipate kile ambacho kwa ajili yake, nimeshikwa na Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Si kwamba nimekwisha kufikia, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha! Bali nakaza mwendo ili nipate kile ambacho kwa ajili yake, nimeshikwa na Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:12
44 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe cho chote kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu.


lakini ijapo iliyo kamili, iliyo kwa, sehemu itabatilika.


Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.


kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo.


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


Illakini, hapo tulipofika na tuenende kwa kanuni ile ile.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo