Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 3:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Ninachotaka tu ni kumjua Kristo na kuiona nguvu ya ufufuo wake, kushiriki mateso yake na kufanana naye katika kifo chake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Ninachotaka tu ni kumjua Kristo na kuiona nguvu ya ufufuo wake, kushiriki mateso yake na kufanana naye katika kifo chake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Ninachotaka tu ni kumjua Kristo na kuiona nguvu ya ufufuo wake, kushiriki mateso yake na kufanana naye katika kifo chake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Nataka nimjue Al-Masihi na uweza wa kufufuka kwake na ushirika wa mateso yake, ili nifanane naye katika mauti yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Nataka nimjue Al-Masihi na uweza wa kufufuka kwake na ushirika wa mateso yake, ili nifanane naye katika mauti yake,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 3:10
34 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, na mtabatizwa ubatizo nibatizwao mimi; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri niwapeni, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.


Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi.


Kama ilivyoandikwa, ya kama, Kwa ajili yako tunauawa mchana kuchwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.


ambae tumemtumainia kwamba atazidi kutuokoa;


Kwa kuwa vile vile kama mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Tangu sasa mtu asinitie taabu; kwa maana ninachiukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.


hatta wote tutakapoufikia umoja wa imani, na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, tuwe watu wakamilifu, hatta cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hayi pamoja nae, akiisba kuwasameheni makosa yote;


BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


Nami naona ni haki, maadam nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsheni kwa kuwakumhusheni.


Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.


Lakiui yeye alishikae neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ilivi twajua ya kuwa tumo ndani yake.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo