Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 hali alijifanya hana utukufu, akitwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wana Adamu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanadamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanadamu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Bali, kwa hiari yake mwenyewe, aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi, akawa sawa na wanadamu, akaonekana kama wanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 bali alijifanya si kitu, akachukua hali hasa ya mtumwa, naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 bali alijifanya si kitu, akachukua hali hasa na mtumwa, naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:7
31 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa?


Maana nani mkubwa, aketiye chakulani, ama akhudumuye?


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


Kwa maana Kristo nae hakujipendeza nafsi yake; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu yalinipata mimi.


Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, nae hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho,


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo