Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, nae hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu; lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kungangania kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu; lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kungangania kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu; lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kung'ang'ania kwa nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa, hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikilia,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa, hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikilia,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:6
37 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Mimi na Baba yangu tu nmoja.


Wayahudi wakamjibu wakinena, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi mawe, bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe, uliye mwana Adamu, wajifanya nafsi yako u Mungu.


lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi, mpate kujua na kuamini ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.


Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Nakwenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi, kwa sababu nashika njia kwenda kwa Baba: kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.


Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


Bassi kwa sababu hii Wayahudi wakazidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na haya alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


Hatta amletapo tena mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, anena, Na malaika wote wa Mungu wamsujudu.


Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.


Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo