Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza wala kujivuna, bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:3
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;


Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana.


Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana.


kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;


mkitumikiana katika khofu ya Kristo.


Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,


Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,


Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.


amejivuna, nae hakufahamu neno lo lote, bali hali yake hali va ugonjwa, kwa khabari ya maswali na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya,


Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo