Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mpokeeni, basi, kwa furaha yote kama ndugu katika Bwana. Mnapaswa kuwastahi watu walio kama yeye,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mpokeeni, basi, kwa furaha yote kama ndugu katika Bwana. Mnapaswa kuwastahi watu walio kama yeye,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mpokeeni, basi, kwa furaha yote kama ndugu katika Bwana. Mnapaswa kuwastahi watu walio kama yeye,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana Isa kwa furaha kubwa, nanyi wapeni heshima watu kama hawa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana Isa kwa furaha kubwa, nanyi wapeni heshima watu kama hawa,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:29
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


Na tulipoondoka wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.


Ikawa furaha kubwa kafika mji ule.


Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema.


illi mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu, mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu, kwa sababu yeye nae amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia na mimi pia.


Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:


Maana wamenihurudisha roho yangu, na roho zenu pia; bassi wajueni sana watu kama hao.


Maana mtu mwenye kubaliwa si yeye ajisifuye, hali yeve asifiwae na Bwana.


Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu, hatukumharibu mtu, hatukumkalamkia mtu.


Nikafanya hidii uyiugi zaidi kumtuma tena, nami nikapunguziwe huzuni yangu.


Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.


Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni;


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo