Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 ijalizeni furaha yangu, illi mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, mkiwa na upendo huo moja, mkiwa wa roho na kusudi moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, mkiwa na upendo huo moja, mkiwa wa roho na kusudi moja.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:2
28 Marejeleo ya Msalaba  

Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake.


HATTA ilipotimia siku ya Pentekote walikuwako wote pamoja mahali pamoja.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani:


Mwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.


Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Nami naliwaandikia neno lili hili, illi, nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumainia ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.


Wala si kwa kuwapo kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu khabari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hatta nikazidi kufurahi.


siku zote killa niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,


nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.


Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakaeangalia hali yenu kweli kweli.


Namsihi Euodia, namsibi na Suntoke, wawe na nia moja katika Bwana.


Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.


Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,


nikikumbuka machozi yako, illi nijae furaha;


Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo waugu katika Kristo.


Nalifurahi mno kwa kuwa naliwaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.


Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo