Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Fanyeni kila kitu bila kunung'unika na bila ubishi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Fanyeni mambo yote bila kunung’unika wala kushindana,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Fanyeni mambo yote bila kunung’unika wala kushindana,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 2:14
36 Marejeleo ya Msalaba  

Wakiisha kupokea, wakamnungʼunikia mwenye nyumba,


maana marhamu hii ingalikuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi wakapewa maskini. Wakamnungʼunikia sana yule mwanamke.


Hatta alipowafikia wanafunzi wake, akaona makutano mengi wakiwazunguka na waandishi wakijadiliana nao;


Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.


Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote.


LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.


Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.


Wala msinungʼunike, kama wengine wao walivyommgʼunika, wakaharibiwa na mharabu.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana.


Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana.


Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;


mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Mwe na amani ninyi kwa ninyi.


Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


kwa maana ghadhabu ya mwana Adamu haiitendi haki ya Mungu.


Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli.


Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.


mwe wakaribishaji ninyi kwa ninyi, pasipo kunnngʼunika;


Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo