Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 1:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Sala yangu ni hii: Naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Sala yangu ni hii: Naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Sala yangu ni hii: naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Haya ndio maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote,

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:9
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


Lakini kama mlivyo na wingi wa vitu vyote, imani, na matamko, na elimu, na bidii yote, na mapenzi yenu kwetu sisi; bassi vivyo hivyo mwe na wingi wa neema hii pia.


Kwa sababu hii msiwe wajinga, bali watu wanaofahamu nini mapenzi ya Bwana.


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.


Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;


ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


illi ushirika wa imani yako ufanye kazi yake katika ujuzi wa killa kitu chema kilicho kwenu katika Kristo Yesu.


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo