Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 1:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Nina hakika ya jambo hili, na hivyo najua kwamba nitaendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili nipate kuongeza maendeleo yenu na furaha katika imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Nikiwa na hakika ya jambo hili, ninajua kwamba nitaendelea kuwepo pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kwa kuwa nina matumaini haya, ninajua kwamba nitaendelea kuwepo na kuwa pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:25
17 Marejeleo ya Msalaba  

lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Na sasa mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowakhubirini ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,


Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa haraka ya Injili ya Kristo.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


bali kudumu katika mwili kwuhitajiwa zaidi kwa ajili yenu.


Maana naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe karibu.


Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo