Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Al-Masihi, na kufa ni faida.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Al-Masihi, na kufa ni faida.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:21
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Kwa maana vyote ni vyenu; ikiwa ni Paolo, au Apollo, au Kefa, au dunia, au uzima, au mauti, au vile vilivyo sasa, au vile vitakavyokuwa,


KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.


Bassi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali ya Bwana.


Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


Illa ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; bassi nitakalolichagua sitambui.


Ninasongwa kati kati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo; maana ni vizuri zaidi;


Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Yesu Kristo.


Kristo atakapoonekana, aliye uzima wetu, ndipo na ninyi mtaonekana pamoja nae katika utukufu.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo