Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Wafilipi 1:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Na huku kuweko kwangu kifungoni kumewafanya ndugu wengi kuwa na imani kwa Bwana, hata wanazidi kuwa hodari katika kuutangaza ujumbe wa Mungu bila hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Na huku kuweko kwangu kifungoni kumewafanya ndugu wengi kuwa na imani kwa Bwana, hata wanazidi kuwa hodari katika kuutangaza ujumbe wa Mungu bila hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Na huku kuweko kwangu kifungoni kumewafanya ndugu wengi kuwa na imani kwa Bwana, hata wanazidi kuwa hodari katika kuutangaza ujumbe wa Mungu bila hofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana Isa wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa sababu ya vifungo vyangu, ndugu wengi katika Bwana Isa wametiwa moyo kuhubiri neno la Mwenyezi Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.


Ya kwamba atatupa sisi, tukiokoka mikononi mwa adui zetu, tumwabudu pasipo khofu,


Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;


Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.


Bassi naomba, msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, yaliyo utukufu kwenu.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.


illi niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.


Tukiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo