Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 6:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Na ninyi, akina bwana, watendeni yayo bayo, mkiacha kuwaogofya, mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, na kwake hapana upendeleo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba nyinyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, naye hatendi kwa ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba nyinyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, naye hatendi kwa ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba nyinyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, naye hatendi kwa ubaguzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Tazama sura Nakili




Waefeso 6:9
40 Marejeleo ya Msalaba  

Watumishi wale wakatoka wakaingia njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema: arusi ikajaa wageni.


Kisha akawaambia watumishi wake. Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.


Bali mtumishi yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;


atamkata vipande viwili, ataweka sehemu yake pamoja na wanafiki: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


Bassi yo yote mtakayo kutendewa na watu, nanyi mwatendee vivyo hivyo: maana hiyo ndiyo torati na manabii.


Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, nanyi watendeeni vivyo hivyo.


Ninyi mwaniita Mwalimu, na Bwana; na mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.


Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;


kwa maana hapana upendeleo kwa Mungu.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


Kwa maana yeye aliyekwitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye nae aliyekwitwa hali ya uhuru, ni mtuniwa wa Kristo.


Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.


NINYI bwana, wapeni watumwa wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.


Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Na huruma hujitukuza juu ya hukumu.


Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema.


Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, uliozuiliwa nanyi kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabaoth.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo