Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 6:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Illakini ninyi nanyi mpate kuyajua mamho yangu ni hali gani, Tukiko, ndugu mpendwa, mkhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisha mambo yote;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu katika kuungana na Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana Isa, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana Isa, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa.

Tazama sura Nakili




Waefeso 6:21
11 Marejeleo ya Msalaba  

Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia.


Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.


Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yamekuja yakaieneza Injili;


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.


Lakini Tukiko nalimpeleka Efeso.


Nitakapomtuma Artema kwako an Tukiko, jitahidi kuja kwangu hatta Nikopoli; maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi.


tokea sasa, si kama mtumwa, baii lieha ya mtumwa, ndugu mpendwa, kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana.


Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.


Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo