Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 6:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Vaeni silaha zote za Mwenyezi Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 6:11
30 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.


maana silaha za vita yetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu kuangusha ngome;


Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.


Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za wema za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto,


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


mkavae mtu mpya, aliyeumbwa kwa namna ya Mungu katika baki na utakatifu wa kweli.


Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kutimiza yote kusimama.


mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.


Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu.


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.


Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo