Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 5:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mchoyo, (ambao ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika ufalme wa Kristo na wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Mwasherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya (mtu kama huyo ni mwabudu sanamu) kamwe hataurithi ufalme wa Al-Masihi na wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Msherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, kamwe hataurithi Ufalme wa Al-Masihi na wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 5:5
15 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.


Na matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasharati, uchafu, ufasiki,


husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.


Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;


aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi.


Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;


Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo