Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 5:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba Mwenyezi kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 siku zote mkimshukuru Mungu Baba kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 5:20
22 Marejeleo ya Msalaba  

Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inakhubiriwa katika dunia yote.


Namshukuru Mungu wangu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;


Ndipo palipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.


wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi; haya hayapendezi; bali afadhali kushukuru.


Namshukuru Mungu wangu killa niwakumbukapo,


Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


Maana shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;


shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,


Bassi na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo ya watu waliungamao jina lake.


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo