Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 5:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo mna upotovu, bali mjazwe Roho wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe Roho.

Tazama sura Nakili




Waefeso 5:18
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa nmasafisha nje ya kikombe na chungu, na ndani yake vimejaa unyangʼanyi na kutoa kuwa na kiasi.


nae akianza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi:


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu?


Bali mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja; akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume na wanawake, na kula na kulewa;


Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,


akamwambia, Killa mtu kwanza huandaa divai iliyo njema, hatta watu wakiisha kunywa sana, ndipo huleta iliyo dhaifu: wewe umeweka divai iliyo njema hatta sasa.


Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


kwa maana killa mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hatta huyu ana njaa, na huyu amelewa.


Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


Maana walalao hulala usiku, na walewao hulewa usiku.


ikiwa mtu hakushitakiwa neno, nae ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni asharati na wasiotii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo