Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 5:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Angalieni sana, bassi, jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio hekima, bali kama wenye hekima;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi. Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa hiyo angalieni sana jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio na hekima, bali kama wenye hekima,

Tazama sura Nakili




Waefeso 5:15
26 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua.


Watano wao walikuwa wenye busara, ua watauo wapumbavu.


Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.


Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.


Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii!


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?


Je! m wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa kwa mwili?


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


Enendeni kwa hekima mbele vao walio nje, mkiukomboa wakati.


Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


Watakao kuwa na mali waanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa zisizo maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wana Adamu katika upotevu na uharibifu.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo