Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 5:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Msishiriki katika matendo yasiyofaa ya giza, bali yafichueni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni.

Tazama sura Nakili




Waefeso 5:11
48 Marejeleo ya Msalaba  

Na ndugu yako akikutenda dhambi, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu: akikusikia, umempata ndugu yako.


Lakini Herode tetrarka, akikaripiwa nae kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo, ndugu yake, na kwa ajili ya maovu yote aliyoyafanya Herode,


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.


Faida gani bassi mliyopata siku zile kwa mambo haya mnayotahayarikia sasa? kwa maana mwisho wa mambo haya ni mauti.


Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele.


mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;


kwa kuwa yanayotendeka nao kwa siri, ni aibu hatta kuyanena.


Bassi msishirikiane nao.


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


Maana walalao hulala usiku, na walewao hulewa usiku.


Na ikiwa mtu aliye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizumgumze nae, apate kutahayarika;


Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.


Wale watendao dhambi, uwakemee mbele ya watu wote, illi na wengine waogope.


Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Nena maneno hayo, ukaonye ukakaripie kwa mamlaka yote; mtu aliye yote asikudharau.


Nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo