Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Mwili mmoja, na Roho moja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:4
28 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Bali twaamini kwamba kwa neema ya Bwana Yesu tutaokoka kama wao.


Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto.


Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.


Lakini sasa viungo ni vingi, na mwili ni mmoja.


Maana yeye ajae akikhubiri Yesu mwingine ambae sisi hatukumkhubiri, au mkipokea Roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumilia nae.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;


Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja.


katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake.


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo