Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Muwe na moyo mwema na wenye kuhurumiana; kila mmoja na amsamehe mwenzake kama naye Mungu alivyowasamehe nyinyi kwa njia ya Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mwenyezi Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:32
34 Marejeleo ya Msalaba  

Utusamehe deni zetu, kama sisi tunavyowasamehe wadeni wetu.


Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.


Kwa rehema zake Mungu wetu, Kwazo mwangaza wa juu umetujia,


Utupe leo riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi nasi tunamsamehe killa mtu anaewiwa nasi. Usituingize majaribuni, hali utuokoe na yule mwovu.


na akikosa marra saba katika siku moja, akakurudia marra saba, akisema, Natubu, msamehe.


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


msipatilize, nanyi hamtapatilizwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.


Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni,


Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,


hatta, kiuyume cha hiyo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyu asije akatoswa katika huzuni ipitayo kiasi.


katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki,


BASSI mwe wafuasi wa Mungu, kama watoto wanaopendwa;


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.


Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo