Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Uchungu wote na hasira na ghadhabu na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na killa ubaya;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Basi, achaneni na uhasama, chuki, hasira, kelele na matusi. Acheni kila uovu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu na hasira, makelele na masingizio, pamoja na kila aina ya uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:31
62 Marejeleo ya Msalaba  

Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paolo, wakamwokota, wakamtoa hekaluni; marra milango ikafungwa.


Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


bassi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochacha, ndio weupe wa moyo na kweli.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,


mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;


Bassi uvueni uwongo, mkaseme kweli killa mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, killa mmoja kiungo cha wenzake.


Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni;


Ninyi waume, wapendeni wake zenu, msiwe na uchungu nao.


Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.


Vivi hivi wanawake wawe watu wa utaratibu, si wasingiziaji, watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.


si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha;


Na pamoja na hayo wajifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi, hujishughulisha na mambo ya wengine wakinena maneno yasiyowapasa.


Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:


wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli.


Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.


BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote,


si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki.


Killa amchukiae ndugu yake ni mwuaji: nti mnajua ya kuwa mwuaji bana uzima wa milele ukikaa ndani yake.


Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo