Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba nyinyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:30
23 Marejeleo ya Msalaba  

Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili:


Bassi hayo yaanzapo kuwa, tazameni juu, mkainue vichwa vyenu kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.


Aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri yake kwamba Mungu ni kweli.


Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya na ninyi vivyo hivyo.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Wala si hivyo tu, illa na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho tunaugua katika nafsi zetu, tukitazamia kufanywa wana, ukombozi wa mwili wetu.


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu;


Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo