Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yanayofaa kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:29
41 Marejeleo ya Msalaba  

Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf?


Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu akageuka, akawaona wakifuata: akawaambia, Mnatafuta nini?


Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.


Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe.


lakini napenda kunena maneno matano katika kanisa kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno elfu kumi kwa lugha.


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa, kwa msaada wa killa kiungo, kwa kadiri ya kazi ya killa sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.


Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.


Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe;


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo