Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, apafe kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kinachofaa kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:28
33 Marejeleo ya Msalaba  

Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne.


Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.


Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.


Maana wengine, kwa kuwa Yuda aliuchukua mfuko, walidhani ya kuwa Yesu alimwambia, Nunua tunavyovihitaji kwa siku kuu; au kwamba awape maskini kitu.


kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.


tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


maana walipokuwa wakijaribiwa kwa shidda nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa unyofu wao.


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo,


Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema kwa matumizi yaliyo lazima, illi wasiwe hawana matunda.


Neno hili ni amini, na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, illi wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Haya ni mazuri, tena yana faida kwa wana Adamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo