Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 mkavae mtu mpya, aliyeumbwa kwa namna ya Mungu katika baki na utakatifu wa kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 na mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki ya kweli na utakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mwenyezi Mungu katika haki yote na utakatifu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:24
30 Marejeleo ya Msalaba  

Katika utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote.


Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


Bassi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tutembee katika upya wa uzima.


Bali sasa tumetolewa katika torati isitukhusu kitu, tumeilia hali ile iliyotupinga, tupate kutumika sisi katika hali mpya chini ya roho, si katika hali ya zamani, ya dini ya sharia iliyoandikwa.


Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi.


Maana sharti huu wenye uharibifu uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.


Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.


akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani;


Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, illi kwa hayo mpate kunkulia wokofu;


kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo