Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 watu waliopooza kabisa, wamejitia katika mambo ya ufasiki, wapate kufanyiza killa namna ya uchafu kwa kutamani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Wamepotoka na hawana aibu, wamejitosa katika ufisadi; hufanya kwa pupa kila aina ya mambo ya aibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kujiingiza katika kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:19
13 Marejeleo ya Msalaba  

wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;


Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda wayapendayo mataifa, kuenenda katika uasharati, ua tamaa, na ulevi, ua karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali:


Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni.


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasharati wake, na wafalme wa inchi wamezini nae, na matajiri ya inchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo