Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 4:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, hatutakuwa tena kama watoto, tukitupwa na kupeperushwa huko na huko kwa kila upepo wa mafundisho wanayozua watu wadanganyifu ili wawapotoshe wengine kwa hila.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Basi hatutakuwa tena watoto wachanga, tukiyumbishwa na mawimbi, na tukipeperushwa hapa na pale na kila upepo wa mafundisho, na kwa ujanja na hila za watu katika njama zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 4:14
44 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakienda zao, Yesu akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukilikiswa na upepo?


Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.


Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


kwa maana watu zaidi ya arubaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hatta watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako.


Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.


Ndugu, msiwe watoto katika akili zenu; illakini katika uovu mwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mwe watu wazima.


Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?


Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila zake Shetani.


si mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna, akaanguka katika hukumu ya Shetani.


Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene.


Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.


Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Illa aombe kwa imani, pasipo shaka lo lote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa kwa upepo, na kupeperushwa huko na huko.


Kaziangalieni merikebu; ingawa ni kubwua namna gani, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote aazimuko kwenda yule aongozae.


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo