Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 3:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Injili kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nimekuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa nguvu yake itendayo kazi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 3:7
22 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;


(maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha kwenda kwa mataifa);


na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari,


ikiwa mmesikia khabari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;


Bassi, kwake yeye awezae kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuombayo au tuwazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu,


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa, kwa msaada wa killa kiungo, kwa kadiri ya kazi ya killa sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.


nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu.


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo