Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho wa Mungu kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Siri hii haikudhihirishwa kwa wanadamu katika vizazi vingine kama vile sasa ilivyodhihirishwa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 3:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana amin, nawaambieni, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasivaone; na kuyasikia mnayoyasikia, wasiyasikie.


Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni na ninyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki mtapata.


Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Maana nawaambia; Manabii wengi na wafalme walitaka kuyaona mnayoyatazama ninyi wasiyaone, na kuyasikia mnayoyasikia wasiyasikie.


Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi,


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu.


mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;


na kuwaangaza watu wote, wajue khabari ya kuishiriki siri ile, ambayo tangu zamani zote ilisetirika katika Mungu, aliyeviumba vyote kwa Yesu Kristo:


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo