Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 3:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 na kimjua upendo wake Kristo, ambao hauwezi kufahamiwa vema kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 na kujua upendo huu unaopita fahamu, ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Waefeso 3:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba.


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Ni nani atakaetutenga na upendo wa Kristo, Je! ni shidda, au dhiiki, au adha, au njaa, au uchi, au khatari, au upanga?


wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe cho chote kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu.


Maana upendo wa Kristo watulazimisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, bassi walikufa wote;


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote.


mpale kufahamu pamoja na watakatifu wofe, mapana na marefu na kwenda juu na kwenda chini;


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake,


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


Na amani va Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.


mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo