Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 2:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 naye katika mwili huu mmoja awapatanishe wote wawili na Mwenyezi Mungu kupitia msalaba, ili kwa huo msalaba akaangamiza uadui wao.

Tazama sura Nakili




Waefeso 2:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi.


Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani;


ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;


Mwili mmoja, na Roho moja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu;


akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani;


Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo