Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza, mmekuwa karibu kwa damu ya Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, nyinyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, nyinyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, nyinyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kupitia kwa damu ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini sasa katika Al-Masihi Isa, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mwenyezi Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Waefeso 2:13
41 Marejeleo ya Msalaba  

Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.


Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyekuwa kwenu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakatifu na ukombozi;


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.


kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.


mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;


akatufufua pamoja nae, akatuketisha pamoja nae katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu:


Kwa hiyo hatta lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Tufuate:

Matangazo


Matangazo