Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waefeso 2:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi hamkuwa na tumaini wala Mungu duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 kumbukeni kwamba wakati ule mlikuwa mbali na Al-Masihi, mkiwa mmetengwa kutoka jumuiya ya Israeli, na mkiwa wageni katika yale maagano ya ahadi, nanyi mkiwa hamna tumaini wala Mwenyezi Mungu duniani.

Tazama sura Nakili




Waefeso 2:12
51 Marejeleo ya Msalaba  

Illi kuwatendea rehema baba zetu, Na kukumbuka agano lake takatifu;


Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno.


Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho: kwa kuwa wokofu watoka kwa Wayahudi.


Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu.


Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.


Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.


yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao.


Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.


Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,


akili zao zimetiwa giza, wamekaa mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo niwao, kwa sababu mioyo yao imekufa ganzi:


Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, ua adui katika nia zenu, kwa matendo yemi mabaya, amewapatanisha sasa,


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Lakini, ndugu, hatutaki msijue khabari zao waliolala, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.


si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu;


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


walizima nguvu za moto, waliokoka na ukali wa upanga. Walitiwa nguvu baada va kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.


illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu,


Na killa mwenye kunitumainia hivi hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo