Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 9:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 kana ni hivyo, ingalimpasa kuteswa marra nyingi tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; lakini sasa, marra moja tu, katika mwisho wa dunia, ameonekana, atangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa, nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe tambiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa, nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe tambiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa ulimwengu. Lakini sasa, nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake, yeye ametokea mara moja tu kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewe tambiko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Ingekuwa hivyo, ingempasa Al-Masihi kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Ingekuwa hivyo, ingempasa Al-Masihi kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 9:26
36 Marejeleo ya Msalaba  

na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.


Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Haya yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa illi kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.


LAKINI nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ajapokuwa bwana wa yote;


ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;


Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;


Maana haiyumkini damu ya mafahali na mbuzi iondoe dhambi.


Maana sisi tulioamini tunaingia katika raba ile; kama vile alivyonena, Nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika raha yangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.


asiye na baja killa siku, kwa mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kiisha kwa ajili ya dhambi za watu; maana yeye alifanya hivi marra moja, alipojitoa nafsi yake.


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake.


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo