Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 9:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Maana Kristo hakuingia Mahali Patakatifu palipojengwa kwa mikono ya watu, ambapo ni mfano tu wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni kwenyewe ambako sasa anasimama mbele ya Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Kwa maana Al-Masihi hakuingia patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Kwa maana Al-Masihi hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili yetu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 9:24
32 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


Sisi twalimsikia akiseina, Mimi nitaivunja hekalu hii iliyofanyika kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga ingine isiyofanyika kwa mikono;


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni.


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza?


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


Ni nani atakaewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye awahesabiae haki.


KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.


Nieni yaliyo juu, siyo yaliyo katika inchi.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.


mkhudumu wa patakatifu, na wa khema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwana Adamu.


watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.


BASSI hatta agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidumia.


Bassi sharti manukulu ya mambo yaliyo mbinguni yasafishwe kwa haya, lakini mambo ya mbinguni yenyewe kwa dhabibu zilizo bora kuliko haya.


Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake,


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhbahu, mwenye cheteso cha dhahabu, akapewa manukato mengi illi ayatie pamoja na sala za watakatifu juu ya madhbahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo