Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 9:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Hivyo yeye ni mpatanishi wa agano jipya ambamo wale walioitwa na Mungu wanaweza kupokea baraka za milele walizoahidiwa. Kifo chake huwakomboa watu kutoka yale makosa waliyofanya wakati wa lile agano la kale.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa sababu hii Al-Masihi ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.

Tazama sura Nakili




Waebrania 9:15
52 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.


Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.


Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?


Na mtu mkuhwa mmoja akamwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?


Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.


nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


Kwa maana hapo tulipokuwa sisi hatuna nguvu, wakali ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya maasi.


Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


ndio sisi tulioitwa nae, si watu wa Wayahudi tu, illa watu wa mataifa pia, utasemaje?


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.


Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa kuwa alikuwa hana mkuhwa kuliko nafsi yake wa kumwapia, aliapa kwa nafsi yake,


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


bassi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo hora zaidi.


Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Tufuate:

Matangazo


Matangazo