Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 9:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa kuhani mkuu wa mambo yaliyo mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa kuhani mkuu wa mambo yaliyo mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini Kristo amekwisha fika, akiwa kuhani mkuu wa mambo yaliyo mema, ambayo sasa yamekwisha fika. Yeye anatoa huduma zake katika hema iliyo bora na kamilifu zaidi, isiyofanywa kwa mikono ya watu, yaani isiyo ya ulimwengu huu ulioumbwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Al-Masihi alipokuja akiwa Kuhani Mkuu wa mambo mema ambayo tayari yameshawasili, alipitia kwenye hema iliyo kuu zaidi na bora zaidi, ambayo haikutengenezwa kwa mikono ya binadamu, hii ni kusema, ambayo si sehemu ya uumbaji huu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Al-Masihi alipokuja akiwa Kuhani Mkuu wa mambo mema ambayo tayari yameshawasili, alipitia kwenye hema iliyo kuu zaidi na bora zaidi, ambayo haikutengenezwa kwa mikono ya binadamu, hii ni kusema, ambayo si sehemu ya uumbaji huu.

Tazama sura Nakili

Waebrania 9:11
30 Marejeleo ya Msalaba  

Wewe ndiye ajae, au tumtazamie mwingine?

Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli.

Sisi twalimsikia akiseina, Mimi nitaivunja hekalu hii iliyofanyika kwa mikono, na kwa siku tatu nitajenga ingine isiyofanyika kwa mikono;

Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.

Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi (aitwae Kristo). Atakapokuja yeye, atatufunulia yote.

Illakini yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanyika kwa mikono, kama vile asemavyo nabii:

tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.

KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.

Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;

BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.

Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.

KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,

Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.

KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki;

Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.

Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo