Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 8:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililofanyana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao uiwatoe katika inchi ya Misri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema: “Siku zinakuja, asema Bwana, ambapo nitafanya agano jipya na watu wa Israeli na wa Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema: “Siku zinakuja, asema Bwana, ambapo nitafanya agano jipya na watu wa Israeli na wa Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema: “Siku zinakuja, asema Bwana, ambapo nitafanya agano jipya na watu wa Israeli na wa Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini Mungu aliona kosa kwa watu, naye akasema: “Siku zinakuja, asema Mwenyezi Mungu, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini Mwenyezi Mungu aliona kosa kwa watu, naye akasema: “Siku zinakuja, asema Bwana Mwenyezi, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.

Tazama sura Nakili




Waebrania 8:8
25 Marejeleo ya Msalaba  

maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.


Akawaambia, Hii ni damu yangu, ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya watu wengi.


Akawaambia wanafunzi wake, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku mojawapo ya siku za Mwana wa Adamu wala hamtaiona.


Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.


Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya.


Vivi hivi nacho kikombe baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu: fanyeni liivi killa mnywapo, kwa ukumbusho wangu.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.


bassi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo hora zaidi.


Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.


Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo