Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 8:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Huduma zao za kikuhani ni mfano tu na kivuli cha yale yaliyoko mbinguni. Maana Mose alipokuwa karibu kuitengeneza ile maskani, Mungu alimwambia: “Tengeneza kila kitu kufuatana na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Musa alionywa alipokaribia kujenga Maskani, akaambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano uliooneshwa kule mlimani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni. Hii ndiyo sababu Musa alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: “Hakikisha kuwa unavitengeneza vitu vyote kwa mfano ulioonyeshwa kule mlimani.”

Tazama sura Nakili




Waebrania 8:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.


Ile khema ya shahada ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawa sawa na mfano ule aliouona;


mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


Tuna madhbahu ambayo wale waikhudumiao khema bawana rukhusa kula vitu vyake.


Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake,


Na baada ya haya nikaona, na, tazama, hekalu ya khema ya ushuhuda katika mbingu ilifunguliwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo