Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 8:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Nao hawatafundishana killa mtu na jirani yake, na killa mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watunijua, tangu mdogo wao hatta mkubwa wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake, wala atakayemwambia ndugu yake: ‘Mjue Bwana’. Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mwenyezi,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana.

Tazama sura Nakili




Waebrania 8:11
18 Marejeleo ya Msalaba  

Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu.


Wote wakamsikiliza kwa muda mwingi, tangu mdogo hatta mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni nweza wa Mungu, ule mkuu.


Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo