Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 7:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bali yeye, ambae uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Lakini huyo Melkisedeki hakuwa wa ukoo wa Lawi, hata hivyo alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu; tena akambariki yeye ambaye alikuwa amepewa ahadi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Lakini huyo Melkisedeki hakuwa wa ukoo wa Lawi, hata hivyo alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu; tena akambariki yeye ambaye alikuwa amepewa ahadi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Lakini huyo Melkisedeki hakuwa wa ukoo wa Lawi, hata hivyo alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu; tena akambariki yeye ambaye alikuwa amepewa ahadi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi.

Tazama sura Nakili

Waebrania 7:6
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi m watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.

Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.

ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,

Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa uzao, kana kwamba ni watu wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani Kristo.

Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.

Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaak, awe dhabihu; na yeye aliyezipokea ahadi alikuwa akimtoa mwana wake, mzaliwa wake wa pekee;

KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki;

Na haikanushiki kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo